EUNCCU EUNCCU
UINJILISTI NI UPENDO
Growth ------------------

UINJILISTI NI UPENDO

By @Euticus Nyaga September 28, 2026

Uinjilisti kazi, mwanzilishi ndiye nani? 

Yesu ni mfano wazi, katutuma waumini, 

Kuitilia mizizi, injili tu duniani, 

Uinjilisti kwetu, ni ishara ya upendo. 

Uliyepona tayari, na mwenzao yu gizani, 

Naomba uwe na ari, injili kuihubiri, 

Kamwe usitahayuri, wokovu kuwambieni, 

Uinjilisti kwetu, ni ishara ya upendo. 

Wokovu na tuambie, watilie maanani, 

Kwa Mungu tuwaombee, awanenee rohoni, 

Wokovu wasikatae, Mwokozi na wamwamini, 

Uinjilisti kwetu, ni ishara ya upendo. 

Neno hutuelezea, kuhusu shangwe mbinguni,

 Mtu akimpokea, Mwokozi Yesu moyoni, 

Haifai kulegea, bidii tutilieni, 

Uinjilisti kwetu, ni ishara ya upendo. 

Tamati nimefikia, mema nayaombeeni, 

Enyi mloji tolea, injili kutangazeni, 

Nguvu sijewaishia, Mungu awape amani, 

Uinjilisti pendo, Ee Mungu lidumishe!! 

Share this Article

More Articles

View all